Posts

UBISHI KATI YA KLABU KONGWE TANZANIA NANI KAMFUNGA MWENZAKE ZAIDI UMETATULIWA HAPA

Image
Kila mmoja atakuwa anataka kuona rekodi mpya ikitengenezwa na timu yake anayoipenda na pengine rekodi hiyo idumu kwa muda mrefu ili iendelee kumuumiza mpinzani wake kila inapotokea kubishana kisoka na kunogesha utani wao pindi wanapokutana. Timu hizo mbili zitakuwa zinaingia uwanjani zikiwa narekodo mbili kubwa tofauti na ambazo hutumika kama silaha kwa mshabiki wao katika mazingira ya kutambiana na kuendeleza utamadunia wa jadi katika utani huo. Simba ndio klabu yenye rekodi nzuri ya kuifunga yanga mara nyingi kwa idadi kubwa ya mabao, huku rekodi ya juu kabisa ikiwa ni mwaka 1977 iliposhinda goli 6-0 kichapo kibaya na cha aibu kwa mashabiki wa Yanga na kila wanapokumbushwa kichapo hicho wanakosa namna ya kujitetea kwani katika miaka ya hivi karibuni inaonekana ni vigumu sana Yanga kulipa kisasi hata kama Yanga itakuwa na kikosi bora kiasi gani, lakini mambo huwa yanakuwa magumu kwa upande wao. Ilikuwa Julai 19, mwaka 1977 Simba ikiichapa Yanga goli hizo ambazo zilifungwa ...

Mayanga ataja kikosi cha stars

Image
Leo Mei 19, 2017 kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga ametanga kikosi cha wachezaji watakaoingia kambini kwa ajaili ya mechi ya Juni 10, 2017 dhidi ya Lethoto kuwania kufuzu kucheza fainali za AFCON. Wachezaji walioitwa ni wale wanaocheza Tanzania pamoja na wale wanaokipiga nje ya nchi Magolikipa:  Aishi Manula (Azam FC), Beno Kakolanya (Yanga ) na Said Mohamed ‘Nduda’ (Mtibwa Sugar) Mabeki:  Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Hamisi ‘Kessy’ (Yanga), Mwinyi Haji, (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) Agrey Morris (Azam FC), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC). Viungo:  Himid Mao (Azam FC), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Said Hamisi Ndemla (Simba), Mzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Farid Musa (Tenerife, Hispania), Shiza Kichuya (Simba), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden). Washambuliaji:  Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), Ibrahim Ajib (Simba...

Magazeti ya ulaya leo 19.05.2017

Image
The Sun.Crystal Palace wanaangalia uwezekano wa kuwanunua Bacary Sagna na Gael Clichy ambao wote mikataba yao inakaribia kikomo Manchester City, kinda wa Kisenegal mwenye miaka 18 Mamadou Coulibaly amepata bahati kutoka katika maisha ya ukimbizi hadi kuichezea Juventus. The Sun tena linasema Antonio Conte yuko katika mpango wa kumnunua Pierre Aubemayang ili kuziba pengo la Diego Costa endapo ataondoka Chelsea,na mshambuliaji Ashley Barnes wa Burnley anaweza kujiunga na Crystal Palace au Newcastle ambazo zote zimeonesha kumhitaji. Daily Mail.Claudio Makelele anaweza kupewa nafasi ya kuwepo katika benchi la Swansea baada ya kocha mkuu wa timu hiyo kuamua kuwa na benchi jipya la ufundi, Chelsea na Liverpool zinaweza kumkosa mlinzi wa klabu ya Middlesbrough Ben Gibson baada ya klabu hiyo kusema kuwa hauzwi. Daily Mirror.Manchester United wanapambana vikali kumnunua golikipa Jan Oblak kutokana na kutokuwa na uhakika wa kubaki na David De Gea, huku Crystal Palace nao wameingia kwen...