Mayanga ataja kikosi cha stars



Leo Mei 19, 2017 kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga ametanga kikosi cha wachezaji watakaoingia kambini kwa ajaili ya mechi ya Juni 10, 2017 dhidi ya Lethoto kuwania kufuzu kucheza fainali za AFCON.
Wachezaji walioitwa ni wale wanaocheza Tanzania pamoja na wale wanaokipiga nje ya nchi
Magolikipa: Aishi Manula (Azam FC), Beno Kakolanya (Yanga ) na Said Mohamed ‘Nduda’ (Mtibwa Sugar)
Mabeki: Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Hamisi ‘Kessy’ (Yanga), Mwinyi Haji, (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) Agrey Morris (Azam FC), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).
Viungo: Himid Mao (Azam FC), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Said Hamisi Ndemla (Simba), Mzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Farid Musa (Tenerife, Hispania), Shiza Kichuya (Simba), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden).
Washambuliaji: Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), Ibrahim Ajib (Simba) na Abdulrahman Musa (Ruvu Shooting).
Wachezaji wataingia kambini Mei 23, 2017 na kuanza mazoezi Mei 24 hadi 29, Mei 30, 2017 kikosi kizima kitasafiri kwenda Misri kwa kambi ya siku saba. Juni 7, 2017 timu itarejea Dar na kufanya mazoezi kwa siku mbili kabla ya mchezo unaotarajia kuchezwa juni 10 mwaka huu.
Wachezaji wa Simba watajiunga na kambi Mei 29,  baada ya mechi yao ya fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC mechi iliyopangwa kuchezwa Mei 27, mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Wachezaji wote wanaocheza nje ya nchi watajiunga na timu Misri June 1, 2017 ikiwa ni baada ya kalenda ya FIFA kuruhusu wachezaji wa vilabu kujiunga na timu zao za taifa kwa ajili ya mechi mbalimbali.

#SJ11

Comments

Popular posts from this blog

UBISHI KATI YA KLABU KONGWE TANZANIA NANI KAMFUNGA MWENZAKE ZAIDI UMETATULIWA HAPA

Simba washikwa mkia naona jinsi watakavyo anguka tena