UBISHI KATI YA KLABU KONGWE TANZANIA NANI KAMFUNGA MWENZAKE ZAIDI UMETATULIWA HAPA
Kila mmoja atakuwa anataka kuona rekodi mpya ikitengenezwa na timu yake anayoipenda na pengine rekodi hiyo idumu kwa muda mrefu ili iendelee kumuumiza mpinzani wake kila inapotokea kubishana kisoka na kunogesha utani wao pindi wanapokutana.
Timu hizo mbili zitakuwa zinaingia uwanjani zikiwa narekodo mbili kubwa tofauti na ambazo hutumika kama silaha kwa mshabiki wao katika mazingira ya kutambiana na kuendeleza utamadunia wa jadi katika utani huo.
Simba ndio klabu yenye rekodi nzuri ya kuifunga yanga mara nyingi kwa idadi kubwa ya mabao, huku rekodi ya juu kabisa ikiwa ni mwaka 1977 iliposhinda goli 6-0 kichapo kibaya na cha aibu kwa mashabiki wa Yanga na kila wanapokumbushwa kichapo hicho wanakosa namna ya kujitetea kwani katika miaka ya hivi karibuni inaonekana ni vigumu sana Yanga kulipa kisasi hata kama Yanga itakuwa na kikosi bora kiasi gani, lakini mambo huwa yanakuwa magumu kwa upande wao.
Ilikuwa Julai 19, mwaka 1977 Simba ikiichapa Yanga goli hizo ambazo zilifungwa na Abdallah ‘King’ Kibadeni aliyekuwa mwiba mchunga zaidi siku hiyo kwani alifunga magoli matatu maarufu kama ‘hat-trick’ katika dakika za 10, 42 na 89.
Mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Cosmopolitan, Jumanne Hassan ‘Masimenti’ alifunga mabao mawili katika dakika za 60 na 73 na kutokana na ‘kiwewe’ cha Yanga siku hiyo, Selemani Sanga alijifunga katika dakika ya 20.
Yanga alimfunga Simba 5-0 june 1968 kabla ya Simba kulipiza kisasi Julai 77 kwa ushindi mnono zaidi wa magoli 6-0. Simba ikapata ushindi wa 3-1 Oktoba 1979 na kurejea tena ushindi wa 3-0 Oktoba 1980 kabla ya Yanga kulipa kisasi Septemba 1982 na April 1983 kwa ushindi wa 3-1.
Oktoba mwaka 1990 Yanga akaibuka tena na ushindi wa 3-1 na tangu hapo ni Simba aliyeendelea kutamba kwa ushindi wa zaidi ya goli tatu, Julai 1994 Simba alichomoza na ushindi wa 4-1, akarejea tena April 2010 kwa ushindi wa 4-3 kabla ya Mei 2012 ilipochomoza na ushindi wa 5-0 mchezo ambao Yanga walikumbushwa maumivu ya mwaka 1977 ya kichapo cha 6-0.
Kwa Takwimu hizi ni wazi kwamba Simba amekuwa na rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi katika mchezo mmoja zaidi ya Yanga.
IFUATAYO NI REKODI YA MATOKEO YA MICHEZO YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA TANGU MWAKA 1955 (ZINGATIA NI MICHEZO YA LIGI TU)
MACHI 30, 1955
Yanga v/s Sunderland, 1-0
MFUNGAJI: Kitwana Manara dk 28.
Yanga v/s Sunderland, 3-2
WAFUNGAJI:
Yanga: Abdulrahim Lukongo dk 54, Andrew Tematema dk 67, Emmanuel Makaidi dk 83.
Sunderland: Mustafa Choteka dk 24, Haji Lesso dk 86.
NOVEMBA 26, 1966
Sunderland v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Mustafa Choteka dk 44.
JUNI 1, 1968
Yanga v/s Sunderland, 5-0
WAFUNGAJI: Maulid Dilunga dk 18 (Penalti), Dilunga dk 43, Saleh Zimbwe dk 54, Zimbwe dk 89 na Kitwana Manara dk 86.
MACHI 3,1969
Yanga v/s Sunderland
(Yanga ilipewa ushindi baada ya Sunderland kugoma kucheza).
JUNI 4, 1972
Yanga v/s Sunderland, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Kitwan Manara dk 19
Sunderland: Willy Mwaijibe dk 11.
JUNI 18, 1972
Yanga v/s Sunderland, 1-0
MFUNGAJI: Leonard Chitete.
JUNI 23, 1973
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Haidari Abeid ‘Muchacho’ dk 68.
AGOSTI 10, 1974
Yanga v/s Simba, 2-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Gibson Sembuli dk 87, Sunday Manara dk ya nyongeza)
Simba: Adam Sabu dk 16.
(Uwanja wa Nyamagana, Mwanza)
JULAI 19, 1977
Simba v/s Yanga, 6-0
WAFUNGAJI: Abdallah Kibaden dk 10, 42 na 89, Jumanne Hassan dk 60, 73 na Seleman Sanga aliyejifunga dk 20.
OKTOBA 7, 1979
Simba v/s Yanga, 3-1
WAFUNGAJI:
Simba: Nico Njohole dk 3, Mohamed Bakari ‘Tall’ dk 38, Abbas Dilunga dk 72.
Yanga: Rashid Hanzuruni.
OKTOBA 4, 1980
Simba v/s Yanga, 3-0
WAFUNGAJI: Abdallah Mwinyimkuu dk 29, Thuwein Ally dk 82, Nico Njohole dk 83.
SEPTEMBA 5, 1981
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Juma Hassan Mkambi dk 42.
APRILI 29, 1982
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Rashid Hanzuruni dk 2.
SEPTEMBA 18, 1982
Yanga v/s Simba, 3-0
WAFUNGAJI: Omar Hussein dk 2 na 85, Makumbi Juma dk 62.
FEBRUARI 10, 1983
Yanga v/s Simba, 0-0
APRILI 16, 1983
Yanga v/s Simba, 3-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Charles Boniface Mkwasa dk 21, Makumbi Juma dk 38, Omar Hussein 84,
Simba: Kihwelo Mussa dk 14.
SEPTEMBA 10, 1983
Yanga v/s Simba, 2-0
WAFUNGAJI: Lila Shomari alijifunga dk 72 na Ahmed Amasha dk 89.
SEPTEMBA 25, 1983
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Makumbi Juma dk 75
Simba: Sunday Juma dk 72.
MACHI 10, 1984
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Omar Hussein dk 72
Simba: Idd Pazi kwa penalti dk 20.
JULAI 14, 1984
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Abeid Mziba dk 39
Simba: Zamoyoni Mogella dk 17.
MEI 19, 1985
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Omar Hussein dk 6
Simba: Mohammed Bob Chopa dk 30.
AGOSTI 10, 1985
Yanga v/s Simba, 2-0
MACHI 15, 1986
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Abeid Mziba dk 44
Simba: John Douglas dk 20.
AGOSTI 23, 1986
Simba v/s Yanga, 2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Edward Chumila dk 9, Malota Soma dk 51
Yanga: Omar Hussein dk 5.
JUNI 27, 1987
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Edgar ‘Fongo’ Mwafongo dk 36.
AGOSTI 15, 1987
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Abeid Mziba dk 14.
APRILI 30, 1988
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Justin Mtekere dk 28
Simba: Edward Chumila dk 25.
JULAI 23, 1988
Simba v/s Yanga, 2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Edward Chumila dk 21, John Makelele dk 85.
Yanga: Issa Athuman dk 36.
JANUARI 28, 1989
Yanga v/s Simba, 2-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Issa Athuman dk 4, Abeid Mziba 85,
Simba: Malota Soma dk 30.
MEI 21, 1989
Yanga v/s Simba, 0-0
MEI 26 1990
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Mavumbi Omari dk 6
OCTOBA 20, 1990
Yanga v/s Simba, 3-1
WAFUNGAJI:
Yanga; Makumbi Juma dk 33, Thomas Kipese dk 82, Sanifu Lazaro.
Simba; Edward Chumila dk 58.
MEI 18, 1991
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Said Sued ‘Scud’ dk 7
AGOSTI 31, 1991
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Said Sued ‘Scud’
OKTOBA 9, 1991
Yanga v/s Simba, 2-0
WAFUNGAJI: Athuman China dk 3, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ dk 54.
NOVEMBA 13, 1991
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Kenneth Mkapa dk 10.
SEPTEMBA 26, 1992
Yanga v/s Simba, 2-0
OCTOBA 27, 1992
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Damian Kimti.
MACHI 27, 1993
Yanga v/s Simba, 2-1
WAFUNGAJI:
Yanga; Said Mwamba ‘Kizota’ dk 47 na 57
Simba; Edward Chumila
JULAI 17, 1993
Simba v/s Yanga 1-0
MFUNGAJI: Dua Said dk 69.
SEPTEMBA 26,1993
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Dua Said dk 13.
NOVEMBA 6, 1993
Simba v/s Yanga, 0-0
FEBRUARI 26, 1994
Yanga v/s Simba, 2-0
WAFUNGAJI: Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ na James Tungaraza ‘Bolizozo’.
JULAI 2, 1994
Simba v/s Yanga, 4-1
WAFUNGAJI:
Simba; George Masatu, Athuman China, Madaraka Seleman na Dua said
Yanga; Costantine Kimanda.
NOVEMBA 2, 1994
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Madaraka Selemani dk 71.
NOVEMBA 21, 1994
Simba v/s Yanga, 2-0
WAFUNGAJI: George Lucas dk 18, Madaraka Selemani dk 42.
MACHI 18, 1995
Simba v/s Yanga, 0-0
OKTOBA 4, 1995
Simba v/s Yanga, 2-1
WAFUNGAJI:
Simba; Said Mwamba ‘Kizota’ dk 70, Mchunga Bakari dk 79
Yanga; Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ dk 40.
FEBRUARI 25, 1996
Yanga v/s Simba, 2-0
SEPTEMBA 21, 1996
Yanga v/s Simba, 0-0
OKTOBA 23, 1996
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ dk 46
NOVEMBA 9, 1996
Yanga v/s Simba, 4-4
WAFUNGAJI:
Yanga; Edibiliy Lunyamila (Penalti) dk 28, Mustafa Hoza alijifunga dk 64, Said Mwamba dk 70, Sanifu Lazaro dk 75
Simba; Thomas Kipese dk 7, Ahmed Mwinyimkuu dk 43, Dua Said 60 na 90.
APRILI 26, 1997
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga; Idelfonce Amlima dk 16
Simba; Abdallah Msamba dk 1.
AGOSTI 31, 1997
Yanga v/s Simba, 0-0
OCTOBA 11, 1997
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga; Sekilojo Johnson Chambua dk 52
Simba; George Masatu dk 89.
NOVEMBA 8, 1997
Yanga v/s Simba, 1-0
MFUNGAJI: Sekilojo Johnson Chambua dk 85.
FEBRUARI 21, 1998
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Akida Makunda dk 46
Simba: Athuman Machepe dk 88.
JUNI 7, 1998
Yanga v/s Simba, 1-1
WAFUNGAJI:
Yanga; Idelfonce Amlima dk 28
Simba; Abuu Juma (Penalti) dk 32.
MEI 1, 1999
Yanga v/s Simba, 3-1
WAFUNGAJI:
Yanga; Idd Moshi dk 59, Kalimangonga Ongala dk 64, Salvatory Edward 70,
Simba; Juma Ameir Maftah dk 12.
AGOSTI 29, 1999
Yanga v/s Simba, 2-0
WAFUNGAJI: Bakari Malima dk 49, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ dk 71.
JUNI 25, 1999
Simba v/s Yanga, 2-1
WAFUNGAJI:
Simba; Steven Mapunda dk 59 na 72
Yanga; Idd Moshi dk 4.
AGOSTI 5, 2000
Yanga v/s Simba, 2-0
WAFUNGAJI: Idd Moshi dk 37 na 47
SEPTEMBA 1, 2001
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Joseph Kaniki dk 76.
SEPTEMBA 30, 2001
Simba v/s Yanga, 1-1
WAFUNGAJI:
Simba; Joseph Kaniki dk 65
Yanga; Sekilojo Chambua dk 86.
AGOSTI 18, 2002
Simba v/s Yanga, 1-1
WAFUNGAJI:
Simba; Madaraka Seleman dk 65
Yanga; Sekilojo Chambua (Penalti) dk 89.
NOVEMBA 10, 2002
Simba v/s Yanga, 0-0
SEPTEMBA 28, 2003
Simba v/s Yanga, 2-2
WAFUNGAJI:
Simba; Emmanuel Gabriel dk 27 na 36
Yanga; Kudra Omary dk 42, Henry Morris dk 55.
NOVEMBA 2, 2003
Simba v/s Yanga, 0-0
AGOSTI 7, 2004
Simba v/s Yanga, 2-1
WAFUNGAJI:
Simba; Shaaban Kisiga dk 64, Ulimboka Mwakingwe dk 76,
Yanga; Pitchou Kongo dk 48.
SEPTEMBA 18, 2004
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Athumani Machuppa dk 44.
APRILI 17, 2005
Simba v/s Yanga, 2-1
WAFUNGAJI:
Simba; Nurdin Msiga dk 44, Athuman Machuppa dk 64
Yanga; Aaron Nyanda dk 39.
AGOSTI 21, 2005
Simba v/s Yanga, 2-0
WAFUNGAJI: Nico Nyagawa dk 22 na 56.
MACHI 26, 2006
Simba v/s Yanga, 0-0
OKTOBA 29, 2006
Simba v/s Yanga, 0-0
JULAI 8, 2007
Simba v/s Yanga, 1-1
WAFUNGAJI:
Simba; Moses Odhiambo (Penalti) dk 2
Yanga; Said Maulid dk 55.
(Mchezo huo ulikuwa wa fainali ya Ligi Ndogo ya TFF. Ulimaliza dakika 120 na kuamuliwa kupigwa penalti na Simba ilishinda kwa 5-4).
OKTOBA 24, 2007
Simba v/s Yanga, 1-0
MFUNGAJI:
Simba: Ulimboka Mwakingwe dk 32.
APRIL 27 2008
Simba vs Yanga, 0-0
Oktoba 26 2008
Simba 0 Yanga 1
Mfungaji Ben Mwalala dk 16
April 26 2009 Marudinao
Yanga vs Simba, 2-2
Wafungaji Simba Ramadhan Chombo ‘Redondo dk Haruna Moshi Boban dk
Yanga Ben Mwalala dk Jerry Tegete dk
Yanga Ben Mwalala dk Jerry Tegete dk
OKTOBA 31, 2009
Simba Vs Yanga, 1-0
MFUNGAJI: Mussa Hassan Mgosi dk 26
(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)
(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)
APRILI 18, 2010
Simba Vs Yanga, 4-3
WAFUNGAJI: SIMBA: Uhuru Suleiman dk 3, Mussa Mgosi dk 53 na 74, Hillary Echesa dk 90+
YANGA: Athumani Iddi dk 30, Jerry Tegete dk 69 na 89
YANGA: Athumani Iddi dk 30, Jerry Tegete dk 69 na 89
OKTOBA 16, 2010:
Yanga Vs Simba, 1-0
MFUNGAJI: Jerry Tegete dk 70
MACHI 5, 2011
Simba Vs Yanga, 1-1
WAFUNGAJI: YANGA: Stefano Mwasyika (penalti) dk 59.
SIMBA: Mussa Mgosi dk 73.
SIMBA: Mussa Mgosi dk 73.
OKTOBA 29, 2011
Yanga 1-0 Simba.
MFUNGAJI: Davies Mwape dakika ya 75
MEI 6, 2012
Simba 5-0 Yanga
WAFUMNGAJI: Emmanuel Okwi dk 1 na 65, Patrick Mafisango pen dk 58, Juma Kaseja pen dk 69 na Felix Sunzu pen dk 74
Oktoba 3 2012
Yanga vs Simba, 1-1
WAFUNGAJI: Amri Kiemba DK 3, Yanga Saidi Bahanuzi Dk 64
Mei 18 2013
Yanga vs Simba, 2-0
Wafungaji: Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza
Oktoba 20 2013
Simba vs Yanga, 3-3
Wafungaji wa Yanga: Mrisho Ngasa dk 14 na Mganda Hamisi Kiiza aliyefunga mara mbili dakika ya 35,47
Mabao ya Simba: Beatram Mwombeki dakika ya 53, Joseph Owino dakika ya 5 na Mrundi Gilbert Kaze dakika ya 83
(mechi hii ikiwa maalumu ikipewa jina la Nani Mtani Jembe).
(mechi hii ikiwa maalumu ikipewa jina la Nani Mtani Jembe).
April 19 2014
Yanga vs Simba, 1-1
Wafungaji:Simba Haruna Chanongo dk 76 Yanga Simon Msuva dk 86
Oktoba 18 2014
Simba vs Yanga, 0-0
Machi 08 2015
Yanga vs Simba, 0-1
Mfungaji: Emmanuel Okwi dakika ya 52.
2015/2016 yanga walishinda mechi zote mbili kwa magoli 2 kwa 0
2016/17 mechi ya kwanza imeisha kwa droo ya 1 1 na ya pili simba 2 yanga 1
2015/2016 yanga walishinda mechi zote mbili kwa magoli 2 kwa 0
2016/17 mechi ya kwanza imeisha kwa droo ya 1 1 na ya pili simba 2 yanga 1
Timu hizi zimefkisha michezo 84 kwa timu hizo kukutana katika ligi kuu tangu ilipoanzishwa mwaka 1965 wakati huo ikiitwa ligi ya taifa.Yanga imekuwa na matokeo ya ushindi mara nyingi zaidi ikilinganishwa na watani zao Simba kwa kushinda michezo 31 huku Simba ikipata ushindi mara 24na sare katika michezo 29( Zingatia kuwa hii ni michezo ya ligi pekee).
Yanga imefunga jumla ya magoli 92 na Simba magoli 78, hivyo Simba inahitaji magoli 14 ya kutengeneza uwiano sawa wa magoli ya kufungana (Utafiti huu umefanywa na mwandishi mkongwe wa michezo hapa nchini Brother Daniel Mbega kupitia kitabu chake cha SIMBA VS YANGA: VUTA-NIKUVUTE’).
Sj11
Sj11
Comments
Post a Comment