INAWEZEKANA ni kweli mlinzi wa kati wa Kagera Sugar FC, Mohamed Fakhi alicheza mchezo wa Kagera 2-1 Simba SC akiwa na kadi tatu za njano, lakini Shirikisho la Soka nchini-TFF wamewapa Simba barua inayoonesha mchezaji huyo hakuwa na kadi tatu za njano-ambazo Simba wanadai ilikuwa hivyo. MALALAMIKO YASIYO NA MASHIKO FIFA Simba wamepeleka malalamiko yao FIFA wakiwa na nakala ya barua kutoka TFF ambayo wanadai haikuwatendea haki. Ieleweke Simba wameenda FIFA wakiwa na barua ambayo inaonyesha ‘mchezaji anayelalamikiwa ’ hakuwa na kadi tatu za njano. Kwa hiyo wanachojaribu kufanya viongozi wa Simba hivi sasa ni kuendelea kuwahadaa wanachama wao kwa sababu makosa ni yao wenyewe. Inawezekana makosa yasiwe yale ya kupoteza mchezo wa Kagera sababu bahati nzuri hawajanyang’any wa ushindi wao, bali wanapigania ushindi ambao hawakuupata ndani ya dakika 90. Kama unaona mbali katika hili unaweza kuona malalamiko ya Simba waliyopeleka FIFA hayana ‘mashiko,’ na nachokiona ni muendelezo wa u...