Simba kukutana na raisi magufuli

Wazee wa klabu ya Simba wameomba kukutana na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kufikisha kilio chao kuhusu watu wanaotaka kuichukua klabu yao.

Mzee Felix Mapua amesema, tayari wamemwandikia barua Rais Magufuli kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

“Sisi wazee kupitia kikao chetu cha juzi Mei 15, 2017 tuliazimia mambo kadhaa, jambo la kwanza ni kuomba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli barua yetu tumeiandika jana kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.”

“Tunaamini Rais wetu ni msikivu, mwenye huruma, kutenda haki na kimbilio la wanyonge. Sasa hivi klabu yetu imekumbwa na janga kama vile alivyoingia Nduli Idd Amini ndio Nduli alivyoingia katika klabu yetu anataka aichukue klabu yetu pamoja na mali zake. Sakata hili tumehangaika nalo kwa kipindi kirefu lakini sasa hivi limefika pabaya baada ya kugundua kwamba mbali na viongozi wa Simba kutumia hila hizo lakini kuna baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali wameshirikishwa katika kuipoka klabu ya Simba.”

“Tunamuomba Rais wetu tumueleze kinaga ubaga na kumtajia genge linaloshiriki kuipoka klabu ya Simba inayoundwa na wanachama sio kwa nia ya kumkodisha mtu, tunachoruhusu ni udhamini kama wadhamini wetu wa sasa.”

“Kama serikali itashindwa kutusikiliza, plan B yetu ni kwenda mahakama kuu na tayari tuna mawakili sita ambao wako tayari kutusaidia kwenye kesi hii.”

“Rais wetu ni msikivu wa wanyonge tukamuelezee ili aweze kutusaidia, sasa hivi tumemuomba Waziri mwenye dhamana asitishe huu mpango kwa sababu tayari tumeshaupeleka TAKUKURU na tayari baadhi ya wanachama wameanza kuhojiwa nikiwemo mimi na juzi amehojiwa Rais wa Simba Evans Aveva.”

#sj11

Comments

Popular posts from this blog

UBISHI KATI YA KLABU KONGWE TANZANIA NANI KAMFUNGA MWENZAKE ZAIDI UMETATULIWA HAPA

Simba washikwa mkia naona jinsi watakavyo anguka tena